Powered by Blogger.

On Bloggers

WIZARA YA HABARI YAZINDUA BODI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

  Na Dotto Kwilasa,Dodoma Wizara  ya Habari,Mawasilino na Teknolojia ya Habari imezindua Bodi ya tume ya ulinzi wa taarifa binafsi huku ikiw...

 


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Wizara  ya Habari,Mawasilino na Teknolojia ya Habari imezindua Bodi ya tume ya ulinzi wa taarifa binafsi huku ikiwataka wajumbe wa Bodi hiyo kuendeleza historia ambayo inakwenda kutengeneza jamii ya watu wastarabu kwa kuanzishwa tume hiyo. 

Waziri mwenye dhamana hiyo Nape Nnauye 
akiongea leo January 19,2924 jijini Dodoma kabla ya kuzindua Bodi hiyo amesema ilianza kutungwa sheria ikazaa tume na baadaye ikazaa Bodi ambapo lengo kuu ni kuhakikisha taarifa za watu binafsi zinatunzwa. 

Amesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni taifa salama kwa huduma za kidigitali

"Tume hii ni mpya wenzetu huku mataifa mengine walishaanza na sisi hapa Tanzania Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan na ndio maana akaamua ianzishwe na amefanya kwa imani, "

Na kuongeza kusema "Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata nyinyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya taarifa binafsi nchini ni Bora kuliko tume nyingine duniani, " Amesema Waziri Nnauye

Amesema matumaini ya taifa ni kuona  faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa ,zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa .

"Ninamatumaini baada ya muda watu watakuja kujifunza kwetu juu ya tume hii kwani nchi ya Tanzania ni mwanachama kwa nchi mbalimbali imeanza vizuri hivyo tume kuhakikisha inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na msikubali kuingiliwa na badala yake mlindwe na sheria msiendeshwe, " Amesisitiza Waziri Nnauye 

Na kuongeza "Utoaji wa huduma uhakikishe unaendana na huduma za kidigitali  pia mifumo isomane na iwepo  kila mkoa ili watu watumie mifumo kuliko watu kutoka mikoani kuja Dodoma au Dar es Salaam kutafuta mifumo nasisitiza muweke mifumo inayisomana, " Amesema. 

Kwa Upande Wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdullah alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano

Amesema hayo ni Matokeo ya siku 100 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia 90 kwani wameweza kujenga taasisi yenye sura nzuri inaonekana kujenga utambulisho anuani pamoja na logo na wako kwenye kutengeneza mpango mkakati. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Mohamed Adadi Rajabu wanemshukuru kwa uteuzi wake kwa kuwaaminiwa na kuteuliwa kwenye tume hiyo na ahadi yao ni kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa ili kuhakikisha tume  inafanya kazi vile inavyotakiwa

"Kikubwa ni kuelewa sheria namba 11 inaeleza majukumu ya tume inataka nini, majukumu ya tume inawataka kutunza Siri za watu taarifa za watu binafsi zinatunzwa, " Amesema

Na kuongeza kuwa "Lakini kupitia maaelekezo ya waziri tutafanya kazi vile atakavyoelekeza bila kusahau kutoa uelewa kwa umma ili kujua kazi na majukumu ya tume, "Amesema Mwenyekiti huyo.

COMMENTS

Name

HABARI,6,
ltr
item
MAOKOTO BLOG: WIZARA YA HABARI YAZINDUA BODI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI
WIZARA YA HABARI YAZINDUA BODI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhp0rZxi0JdUtgX70Mb1VxFe0xQ-igIe43pPR6nFk5Xcg9cwG0IB2w2_Vo0ntSFDDP8Bs5WaBOuXLT_EWX7fp6wh0nHWZjbtX_aWF9_IxycZPXdwjhIYPwliRMeAu6aJymaCla8jvjJS79G-qxY3sVwNnfmeIrLA7Hoe15jcAR6o2BVff6ysCR0bHEOLqk/w640-h412/Screenshot_20240119-173408~2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhp0rZxi0JdUtgX70Mb1VxFe0xQ-igIe43pPR6nFk5Xcg9cwG0IB2w2_Vo0ntSFDDP8Bs5WaBOuXLT_EWX7fp6wh0nHWZjbtX_aWF9_IxycZPXdwjhIYPwliRMeAu6aJymaCla8jvjJS79G-qxY3sVwNnfmeIrLA7Hoe15jcAR6o2BVff6ysCR0bHEOLqk/s72-w640-c-h412/Screenshot_20240119-173408~2.jpg
MAOKOTO BLOG
https://maokotoblog.blogspot.com/2024/01/wizara-ya-habari-yazindua-bodi-ya-tume.html
https://maokotoblog.blogspot.com/
https://maokotoblog.blogspot.com/
https://maokotoblog.blogspot.com/2024/01/wizara-ya-habari-yazindua-bodi-ya-tume.html
true
1110674963273841250
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content